Dar es Salaam. Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake watano wamefanikiwa kupata dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Ni baada ya Wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro kuwasilisha cheti kutoka Kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ambapo kimeipa mamlaka mahakama hiyo ya Kisutu kusikiliza kesi hiyo.
Hata hivyo, washtakiwa hao walisomewa mashtaka mapya matano mahakamani hapo leo Ijumaa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa.
Katika mashtaka hayo mawili ni ya kusambaza dawa bandia za kufubaza makali ya ukimwi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, uzembe wa kuzuia kosa kutendeka na kusababisha hasara.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa walikana na wapo nje kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili wanaominika, kila mdhamini akisaini bondi ya Sh 12 milioni.
Pia washtakiwa hao watoe fedha taslimu Sh 12 milioni ama mali isiyo hamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.
0 comments :
Post a Comment