Hatimae Mgombea Ubunge Ccm Jimbo La Nyalandu Apatikana

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale mkoani Lindi, Joseph Monko ameshinda kura ya maoni CCM katika jimbo la Singida Kaskazini.

Ndg Joseph Monko alifanikiwa kupata kura 22 kati ya kura 112 zilizopigwa. Uchaguzi huo uliofanyika katika kijiji cha Ilongera wilayabi Singida ulishirikisha jumla ya wagombea 22.


Uchaguzi huo ulikuwa wa marudio baada ya ule wa awali kufutwa kwa tuhuma za kugubikwa na rushwa.


Mshindi wa pili alikuwa Ndg Choyo Japhet ambaye alipata kura 20. Zoezi la kura za maoni ni sehemu tu ya mchakato wenye lengo la kupata maoni ili kujua mgombea gani anakubalika na kuuzika lakini uteuzi rasmi unafanywa na vikao vya juu vya Chama cha Mapinduzi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment