Mahakama Kuu ya Tanzania imeamuachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Issa Ponda dhidi ya rufaa iliyokatwa na Jamhuri kupinga hukumu ya Mahakama ya Morogoro kumuachia huru kiongozi huyo.
Sheikh Ponda ameachiwa huru leo mbele ya Jaji Johnson Mkasimongwa ambaye amesema anakubaliana na uamuzi wa Mahakama ya Morogoro ya kumuachia huru Sheikh Ponda katika kesi ya kutoa lugha ya uchochezi.
Jaji Mkasimongwa amesema Mahakama ya Morogoro haikukosea kumuachia huru Sheikh Ponda na yeye anakubaliana na uamuzi huo, hivyo amechukua uamuzi wa kumuachia huru.
Akitolea maelezo juu ya maamuzi hayo, Jaji Mkasimongwa amefafanua kwa kusema kuwa upande Jamhuri haikupaswa kumshtaki Sheikh Ponda kwa kosa lile la kuvunja amri ya Mahakama ya Kisutu bali ilitakiwa wamrudishe katika Mahakama hiyo ili imchukulie hatua zaidi.
Mnamo mwezi August 10, 2013, katika eneo la Kiwanja cha Ndege inadaiwa kwamba Ponda alitoa kauli za kichochezi kwa waumini wa kiislam ambapo moja ya kauli zake alisema kwamba (Waislam) wasikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti, kwa madai kuwa zimeundwa na BAKWATA, ambao ni vibaraka wa CCM na serikali
0 comments :
Post a Comment