Mwanachama wa siku nyingi wa klabu ya Yanga, Ibrahim Akilimali ameshangazwa na wale wanaotaka avuliwe uanachama na kusema hawana jeuri hiyo.
Pamoja na kuibuka na kusema hivyo, Akilimali amesema kama atafanyiwa figisu na kuondolewa Yanga, yeye na wazee wenzake watakwenda hadi ikulu ya Rais Magufuli na kufikisha malalamiko yao.
Leo mchana, baadhi ya wanachama wa Yanga walitaka Akilimali kuondolewa uanachama kwa kuwa amekuwa akizuia mabadiliko ya klabu hiyo.
"Nimezuia mabadiliko yapi, mimi ni kati ya wale tuliotaka mabadiliko hata wengine hawajawa wanachama.
"Tatizo hawa wenzetu wanataka mambo ya haraka na ili mradi kuwaridhisha watu. Lazima tufuate utaratibu na hii ni lazima.
"Kama wanataka kuigawa klabu wanajidanganya na mimi na wazee wenzangu kamwe hatuwezi kukubali," alisema.
0 comments :
Post a Comment