Mgogoro Mwingine Waibuka Anglikana Dar

Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam imemtaka aliyekuwa ofisa ardhi kanisa hilo Kanda ya KinondoniAskofu Oscar Mnung'a kurudisha fedha takriban Sh 8 milioni anazodaiwa baada ya kuuza kiwanja cha kanisa hilo kilichopo Pegwa Kijiji cha Zinga Bagamoyo.
Shamba hilo lililokuwa na miti na matunda linadaiwa kuuzwa mwaka 2013 kwa shirika mojawapo la umma (jina limehifadhiwabaada ya mchakato wa tathimini kukamilika.
Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Desemba 15 kwa vyombo vya habari na Ofisa Habari wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es  Salaam, Yohana Sanga amesema Askofu Mnung'a aliuza kiwanja chenye ekari tano bila lakini hakuweka fedha katika akaunti ya kanisa.
Sanga amesema wamegundua hatua hiyo baada ya kufuatilia kwa wenyeji wa eneo hilo ambao walithibitisha kuuzwa kwa shamba hilo na askofu huyo.
"Baada ya kufutialia kwa kina dayosisi imebaini Askofu Mnung'a alililipwa fedha hizi lakini hakuziwasilisha katika akaunti ya kanisa kama ilivyopaswaKwa mujibu wa maelezo ya mjumbe wa nyumba 10 wa eneo hilo askofu huyo amehusika moja kwa moja katika mchakato huu," amesema Sanga katika taarifa  hiyo.
Kwa mujibu wa SangaAskofu wa Mnung'a hivi yuko dayosisi ya Newala mkoani Mtwara na wanamtaka kuzirudisha fedha hizo na wameamua kutoa taarifa kwa umma baada ya kuona malalamiko ya waumini yanazidi.
Akijibu tuhuma hizo, Askofu Mnung'a alikana na kuhusika na uuzwaji wa kiwanja hicho na kuwataka viongozi wa dayosisi kuwatafuta wahusika wakuu waliouza.
"Katika ile dayosisi kuna matatizo pale hivyo, wanataka kunichafua mimi kwa kunipandikiza mambo yasiyonihusu. Nawaambia wapambane na hali zao mimi simo huko," amesema Askofu Mnung'a.
Askofu Mnung'a aliwataka viongozi  hao wa Dayosisi  ya Dar es Salaam  kuonyesha vielelezo vinavyoonyesha kuwa yeye  alihusika katika mchakato huo wa uuzaji wa kiwanja bila kuwasilisha fedha  katika akaunti ya kanisa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment