Watu tisa wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro wakikabiliwa na shitaka la kumkata mkono albino, Nassoro Mohamed kisha kutoweka na mkono huo.
Washtakiwa hao Anthon Fabian, Jeremia Silwimba, Benard Kifyasi, Joseph Mpeka, Godfrey George, Selemani Mililo, Hassan Zimu, John Fabian na Emanuel Simkonda wote wakazi wa Kijiji cha Nyarutanga Kisaki Wilaya ya Morogoro.
Mbele ya Hakimu, Agripina Kimaze wakili wa serikali Twide Mangula ameeleza kuwa washtakiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo Oktoba 3 mwaka huu katika Kijiji cha Nyarutanga Kisaki Wilaya ya Morogoro na mara baada ya kutenda kosa hilo walikimbia.
Hata hivyo, washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kukosa mamlaka ya kisheria ya kusikiliza kesi hiyo.
0 comments :
Post a Comment