Mugabe Aonekana Hadharani Kwa Mara Ya Kwanza Singapore

Singapore. Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza  tangu awasili wiki hii nchini Singapore kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.
Kiongozi huyo aliyekuwa  madarakani kwa miaka 37 ameonekana akiwa amezungukwa na walinzi wake huku kwa mbele akionekana mwanamke ambaye inaaminika atakuwa mke wake, Grace Mugabe.
Picha za tukio hilo zinamwonyesha akiwa amevalia shati jeupe na suruali nyeusi wakati mtu anayedhaniwa kuwa mke wake akiwa katika vazi jekundu na beki ya mkononi lenye rangi ya zambarau.
Walinzi wake pia wameonekana kuvalia katika hali ya kawaida ikiwa mashati na suruali. Mara nyingi Mugabe pamoja na walinzi wake wa karibu huonekana wakiwa wamevalia suti isipokuwa wakati alipokuwa akishiriki shughuli za chama au katika sherehe za uhuru.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment