Waziri wa habari ,sanaa,utamaduni na Michezo Dr.Harrison Mwakyembe leo amezindua mashindano ya michezo mbalimbali ya Vyuo Vikuu nchini (TUSA) yanayofanyika katika Chuo kikuu Dododma (UDOM).
Katika Uzinduzi huo waziri mwakyembe amesema ,mashindano hayo yanasaidia kubaini vipaji mbalimbali ambavyo vilisahaulika.
"Inatupa Fursa hii michezo kubaini vipaji ambavyo tulishindwa kuviona huko nyuma" . Amesema waziri Mwakyemba.
Pia waziri Mwakyembe amesema mkusanyiko huo utawasaidia wanafunzi kubadilishana mawazo kuhusu masomo yao.
Video hii hapa chini, Dr. mwakyembe wakati anazungumza kwenye uzinduzi huo
Mashindano hayo ambayo kwa mwaka huu jumla ya vyuo 22 vinashiriki kutoa Tanzania bara na Zanzibar yanahusisha michezo ya Mpira wa Miguu,Netball,Volleyball na Basketball.
0 comments :
Post a Comment