Naibu Waziri wa Uvuvi Abdallah Ulega amefanikiwa kukamata tani 11 za Samaki wamagendo katika soko la kimataifa la Samaki Kirumba Mwanza. Samaki hao walikuwa wasafirishwe kwenda nchini DRC kupitia mpaka wa Rusumo Kagera.
Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo shehena ya samaki hao waliokamatwa hawaruhusiwi kuvuliwa kisheria.
Aidha Mh Uledi ameagiza kuondolewa mara moja kwa maofisa uvuvi sokoni hapo kutoka halmashauri ya Manispaa ya wilaya ya Ilemela waliokabidhiwa dhamana ya ukaguzi na ambao walishindwa kuwajibika ipasavyo.
0 comments :
Post a Comment