UONGOZI wa Klabu ya Simba umempatia kiasi cha milioni 50 kiungo wake Mohamed Ibrahim ‘Mo’ kwa ajili ya kuongeza mkataba mpya wa kuitumikia klabu hiyo.
Mo amesaini mkataba wa miaka miwili ya kuitumikia Simba baada ya ule wa awali kufikia tamati ambapo Yanga walikuwa wakimfukuzia.
Taarifa ambazo Championi Jumatatu limezipata ni kwamba kiungo huyo alikubali kuongeza mkataba baada ya kupewa kiasi hicho cha fedha.
Mo ni miongoni mwa wachezaji wenye kiwango katika Klabu ya Simba kutokana na uwezo wake wa kuisaidia timu hiyo katika mechi kadhaa.
“Mo amesajiliwa Simba kwa kiasi cha shilingi milioni 50 baada ya kukubaliana kwa pande zote mbili kutokana na uongozi kukubaliana na kiwango chake .
“Uongozi uliamua kumuongezea kiasi hicho cha fedha kwa lengo la kuzuia usajili mwingine kwa kuwa Yanga walikuwa wakimnyemelea,” alisema mtoa taarifa huyo.
0 comments :
Post a Comment