Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kimewaidhinisha wagombea wawili kuwania kumrithi Rais Jacob Zuma katika uongozi wa chama.
Wagombea hao ni makamu wa rais Cyril Ramaphosa na waziri wa zamani Nkosazana Dlamini-Zuma, mke wa zamani wa bwana Zuma.
Kumekuwa na mvutano, hisia zikipanda, wajumbe wakipiga kelele kupinga taratibu za upigaji wa kura.
Uwaniaji madaraka umeleta mvutano mkubwa wa kisiasa, hali inayoleta hofu kuwa ANC inaweza kugawanyika kabla ya uchaguzi wa 2019.
Rais Zuma ameonya kuwa chama kimo hatarini na kimo kwenye njia panda
Zaidi ya wajumbe 5,000 wanashiriki katika mkutano wa siku nne katika ukumbi wa Expo Centre mjini Johannesburg.
Zaidi ya wajumbe 5,000 wanashiriki katika mkutano wa siku nne katika ukumbi wa Expo Centre mjini Johannesburg.
Kwa namna inavyoonekana, Bw Ramaphosa ana wafuasi 1,469 kulinganisha na 1,094 wa mke wa zamani wa Rais Zuma, Bi Dlamini-Zuma.
Lakini wengi wanasema pale ambapo matokeo yatawekwa wazi, kunaweza kuwa na tofauti nyembamba kabisa kati ya atakayeshinda na atakayeshindwa yatawekwa wazi, anaeleza Lebo Diseko mwandishi wa BBC aliyeko katika eneo la mkutano.
Rais Zuma ambaye amekuwa mamlakani tangu mwaka 2009 anategemewa kusalia uongozini hadi uchaguzi wa taifa mwaka 2019.
Afrika Kusini ina ukomo wa rais kwa vipindi viwili vya miaka mitano.
0 comments :
Post a Comment