TAARIFA KWA UMMA.
Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania wameiuza namba ya simu ya Ben Saanane 0768078523, na sasa inatumika na Mtu mwingine. Vodacom wamefanya hivi wakijua wazi kuwa suala la kupotea kwa Ben bado lipo kwenye uchunguzi. Hii inaweza kuharibu ushahidi juu ya upatikanaji wa Ben.
Taarifa ya LHRC kwa kushirikiana na UTG iliyokwenda umoja wa mataifa (UN) mwezi April mwaka huu imeitaja namba hii kuwa ya Benard Focus Saanane. Taarifa ya UTG kwenda Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora imeitaja namba hii kuwa ya Ben. Jeshi la polisi linaitambua namba hii kuwa ya Ben. Taarifa ya mawasiliano ya Ben kutoka TCRA ilitolewa kwa kutumia namba hii.
Namba hii ni moja ya sehemu muhimu sana Katina uchunguzi wowote unaoendelea kuhusu suala la kupotea kwa Ben. Kuhamisha umiliki wa namba hii kwa mtu mwingine wakati uchunguzi ukiendelea, ni kuharibu ushahidi kwa makusudi.
UTG Tanzania pamoja na familia ya Ben, tunaendelea kutafakari kwa kushirikiana na mawakili wetu kujua hatua mahsusi za kuchukua. Hili walilofanya Vodacom halikubaliki!
Imetolewa na:
Bob Chacha Wangwe
Afisa Mnadhimu Mkuu - UTG
10/12/2017.

0 comments :
Post a Comment