Waziri Atoa Siku 10 Jengo La Tanesco

Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani ametoa siku kumi kwa jengo la  Tanesco lililopo Ubungo libomolewe ili kupisha ujenzi wa barabara ya Morogoro.
Waziri huyo pia  amewataka  watumishi wa Tanesco wanaosimamia jengo hilo na wakandarasi waliowekwa kubomoa jengo hilo wasisafiri wala kusherekea Sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya bali washughulikie jengo hilo kuvunjwa.
 “Nataka kuanzia leo Desemba 22 ndani ya siku sita jengo hili lote libomoke  na kwasababu ni majengo mawili ndani ya siku kumi majengo yote mawili yawe yamebomoka kama mnaona vigumu kubomoa jengo lenu waambieni TBL ”amesema
Amesema  hadi kufikia mwisho wa mwezi huu jengo hilo lote liwe limeanguka chini na hakuna cha sikukuu wala Krisimasi  kwenye kubomoa jengo hili na ujenzi wa barabara kama Tanesco wanaaza waanze tusiwakwamishe”amesema.
Amesema wananchi wameshabomoa majengo yao kwanini Tanesco bado wanasuasua na kudai  Januari mosi ataenda  tena kukagua kuona kama agizo lake limefanyiwa kazi.
“Naimani wananchi hawatapata shida wakati wa sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya ,kwa hiyo asiruhusiwe mtumishi yoyote wa Tanesco kwenda nje ya ofisi yake wakati wa sikukuu zote mbili”amesema
 Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco, Kahitwa Bishaija amesema wamelisikia agizo la Waziri na wataenda kulitekeleza kama lilivyo .
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment