Mamlaka ya Usafiri wa Majini na nchi kavu Tanzania (SUMATRA) imetoa maelezo kwa nini inakusudia kuruhusu mabasi yanayofanya safari zake kwenda mikoani, kufanya safari zake kwa saa 24.
Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv Mkurugenzi wa Barabara SUMATRA Bwn. Johansen Kahatano, amesema wameona kuna uhitaji mkubwa kwa abiria, na kama njia mojawapo ya kupunguza msongamano wa mabasi barabarani.
"Tupo kwenye maandalizi bado hatujaamua, mambo yakikaa sawa sawa tutakwenda na utaratibu huo wa saa 24, ni mahitaji ya wananchi kwamba watu wangependa wafanye kazi muda wote, na matumizi ya magari yenyewe yanaweza yakaenda yakarudi yakaenda, lakini pia kupunguza msongamano wa mabasi pale Ubungo, unaona jinsi hali inavyokuwa muda wa kutoka, sasa ikiwa masaa 24 yatapeana nafasi, na mwisho wa mwaka mabasi baada ya kwenda kulala mahali, yanaendelea na safari zake", amesema Bw. Kahatano.
Hivi karibuni mamlaka hiyo ilikuwa hairuhusu mabasi kufanya safari zake nyakati za usiku kwa kuhofia usalama na ajali za barabarani, wakisema kwamba madereva huwa wanajisahau wanapokuwa barabarani hasa nyakati za usiku.
0 comments :
Post a Comment