Kufuatia barabara, madaraja na mitaro kujaa maji jijini Dar es Salaam kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam, kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (Udart) imesitisha kwa muda huduma za mabasi yake.
Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Januari 8 Mkuu wa mitengo cha mawasiliano wa kampuni hiyo, Deus Bugaywa imesema huduma hizo zitarejea mara baada ya hali kutengamaa.
“Kutokana na maji kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi kwenye barabara ya Morogoro na kusababishwa kufungwa kwa muda kwa barabara hiyo, kampuni ina uarifu umma kuwa huduma za mabasi hayo zimesitishwa kwa muda,” imesema taarifa hiyo na kuongeza,
“Imesitishwa kuanzia saa 3:00 asubuhi, mara baada ya hali kutengemaa na mamlaka husika kuruhusu barabara hiyo kuendelea kutumika, huduma zitarejea mara moja.”
0 comments :
Post a Comment