Baada ya Azam kuingia ‘mchecheto’ na kuomba kubadilishwa mwamuzi wa mechi yao dhidi ya Yanga, kamati ya waamuzi ya TFF imeibuka na kutoa msimamo wake kuhusu ombi la Azam kuelekea mchezo huo utakaochezwa Januari 27, 2018 kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi Salum Umande Chama ametupilia mbali ombi la aza kutaka mwamuzi abadilishwe na badala yeke mwamuzi aliyepangwa kuchezesha mechi hiyo (Israel Mujuni Nkongo) anabaki kuwa mwamuzi atakayepuliza kipyenga katika mchezo huo.
“Jukumu la kupanga waamuzi ni la kamati ya waamuzi wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania na si mtu mwingine yoyote, msimu huu Nkongo ameshachezesha mechi tisa, leo Azam wanamkataa Nkongo kesho Lipuli watamkataa refa wakiwa wanacheza na Ndanda sasa huo hautakuwa mpira kama kila timu inajipangia.”
“Kwa mujibu wa FIFA zipo kazi tisa za kamati ya waamuzi mojawapo ni kupanga waamuzi, nafikiri kama Azam wanalalamika juu ya Nkongo kukoroga mechi, Yanga ndio walipaswa walalamike kwa sababu mechi ya mwisho ambayo ilikuwa na tafrani kati ya Yanga na Azam, Yanga ndio walimfanyia fujo Nkongo sasa sio Yanga wanaolalamika kwa nini Azam walalamike?
“Hatuwezi kuchezesha mpira kama waganga wa kienyeji, lazima tufuate sheria, kanuni na taratibu. Klabu yoyote haiwezi kupanga mwamuzi inaemtaka. Sisi kama shirikiko la mpira wa miguu Tanzania tunasema mwamuzi atakaechezesha mechi hiyo ni Israel Mujuni Nkongo kama wao Azam wanamalalamiko yoyote wacheze wakiwa na pingamizi baada ya mpira kumalizikla tutaangalia kama amekoroga au vinginevyo.”
0 comments :
Post a Comment