Alichozungumza Zitto Baada Ya Kuachiwa Kwa Dhamana


Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Mhe. Zitto Kabwe amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kutoka Mahabusu alikokuwa anashikiliwa toka jana Alhamisi usiku alipokamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Morogoro.
Zitto amesema kukamatwa kwake hakumfanyi asitishe ziara ya Chama cha ACT Wazalendo iliyopagwa kutembelea kata zote zilizo chini ya chama hicho kama walivyotangaza awali.
“Tusirudishwe nyuma na vitisho, usumbufu na sheria kandamizi. Harakati za kulinda Demokrasia yetu na Uhuru wa kukusanyika, kujieleza na kupashana Habari lazima ziendelee. Ni wajibu wetu kulinda Demokrasia ya Vyama vingi na kuiimarisha iwe madhubuti kwa ajili ya Maendeleo ya Watu wetu. Baada ya kulala bure jana polisi Morogoro, tunaendelea na kazi yetu ya kutembelea kata zote ambazo Wananchi walitupa dhamana kwa kuchagua madiwani wa Act Wazalendo,“ameeleza Zitto Kabwe.
Kwa upande mwingine Zitto amelaani mauaji ya Diwani wa CHADEMA huko Ifakara, Morogoro aliyekatwa mapanga na watu wasiojulikana.
“Nawapa pole Wananchi wa Ifakara kwa msiba wa Diwani wao aliyekatwa mapanga mpaka kufa jana Usiku. Nilipata Taarifa hizo nikiwa selo ya Polisi. Mauaji ya namna hii kwa Viongozi wa kisiasa yanatia doa nchi yetu na ni mwendelezo ya uvunjifu mkubwa wa haki za raia.“-amesema Zitto.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment