Kungo wa Manchester United, Paul Pogba, amesema hana furaha kuendelea kuwepo ndani ya Manchester United chini ya Kocha Jose Mourinho.
Kauli hiyo imekuja kufuatia kutotumiwa katika baadhi ya michezo, ikiwemo wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya siku ya Jumatano wiki hii.
Taarifa zinaeleza kukosekana kwa mahusiano mazuri baina ya Mourinho na Pogba, kumefanya wakala wa mchezaji huyo, Mino Raiola, kumtaka Morinho ampe nafasi mchezaji wake la sivyo ataondoka klabuni hapo.
Pogba alisajiliwa na Manchester United akitokea Juventus kwa ada ya dunia, pauni milioni 89.
0 comments :
Post a Comment