Jeshi la Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya wamemkamata mwanamke mmoja mkazi wa 'Airport' ya zamani akiwa na mtoto mchanga jinsia ya kike aliyemuiba katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya.
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi Mohamed .R. Mpinga wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari na kusema mnamo Februari 3, 2018 kwa kushirikiana na viongozi wa hospitali hiyo walifanikiwa kumshika kijana huyo aliyefahamika kwa jina la Happy Charles (24) ambae anajishughulisha na kazi ya Mama lishe.
Aidha, Kamanda Mpinga amesema mnamo Februari mosi mwaka huu majira ya saa 4:00 usiku katika wodi ya watoto Hospitali ya Mkoa wa Mbeya iliyopo Kata ya Forest Mpya, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya, mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Sarah Mwasanga Mkazi wa Iganzo akiwa katika wodi ya wazazi Hospitalini hapo baada ya kujifungua mtoto wa kike aligundua kuibiwa kwa mtoto huyo na mtu asiyefahamika.
Kutokana na tukio hilo, uongozi wa Hospitali hiyo ulitoa taarifa kituo kikuu cha Polisi na ndipo upelelezi kuhusiana na tukio hilo ulianza kufanyika.
Msikilize hapa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi Mohamed .R. Mpinga pamoja na mzazi wa aliyeibiwa mtoto wakifafanua vizuri juu ya tukio hilo.
0 comments :
Post a Comment