Azam Fc Yaweka Kambi Chamazi

Klabu ya soka ya Azam FC imesema haina mpango wa kuweka kambi nje ya uwanja wake wa Azam Complex kwaajili ya kujiandaa na mchezo wake dhidi ya Simba SC.
Msemaji wa klabu hiyo Jaffary Idd amesema kuwa timu imeanza kambi jana Jumapili kwenye makao makuu ya klabu hiyo Chamazinje kidogo ya jiji la Dar es salaam ikiwa ni maandalizi ya mwendelezo wa mechi za ligi ikiwemo ya Simba jumatano.
''Sisi kama Azam hatuna pakwendawala hatutaenda Bagamoyo au Zanzibar zaidi tutakuwepo hapahapa Azam Complex  tutajiandaa na kuondokea hapa kuelekea uwanja wa taifa kwaajili ya mechi''amesema.
Simba na Azam zinakutana katika mchezo wa raundi ya 17 ya ligi kuu soka Tanzania Bara ambapo mchezo wa kwanza utapigwa kwenye dimba la taifa jiji Dar es salaam. Katika mchezo wa raundi ya kwanza kwenye uwanja wa Azam Complex timu hizo zilitoka sare.
Kwa upande mwingine Jaffary Idd amesema kwasasa timu yao ina kikosi kipana licha ya kuwa na majeruhi kadhaa lakini wanaamini waliopo watafanya vizuri. Pia amesema walimu wamelifanyia kazi suala la ufungaji na ndio mana katika mechi zao mbili za mwisho wamefunga mabao nane.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment