Chadema Walimwa Barua Mbili Uchaguzi Kinondoni

Wakati kampeni za uchaguzi jimbo la Kinondoni zikiendelea, Chadema wamepewa barua mbili za malalamiko na  msimamizi  wa uchaguzi Wilaya ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli kikidaiwa kuvunja kanuni za maadili ya uchaguzi.

Akizungumza leo Februari 1, 2018 Mkurugenzi  wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila amesema wamepokea barua hiyo jana, yenye malalamiko yaliyotolewa na Chama cha Wananchi (CUF).

Katika barua hiyo, CUF inalalamika kuwa Januari 28, Chadema walifanya kampeni nyumba kwa nyumba  katika eneo la Kigogo Mbuyuni hadi London Bar badala ya siku hiyo kuwa kata ya Ndugumbi kama ratiba inavyoonyesha.

Malalamiko mengine ni Chadema kudaiwa kutumia salama ya CUF katika majukwaa ya kampeni sambamba na kupamba bendera za chama hicho.

"Madai mengine ni kwamba viongozi  wa CUF  wanakuja katika mikutano yetu  na kukaa meza kuu na kupanda katika majukwaa. Pia CUF wanadai Chadema inawatumia viongozi  wao kupita nyumba kwa nyumba kuiombea kura Chadema  wakiwa na sare za CUF,” amesema Kigaila.

Kwa mujibu wa barua hizo Chadema wanatakiwa kutoa maelezo ya utetezi kwa maandishi  kuhusu tuhuma hizo ndani ya saa 48 baada ya kuzipokea.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment