Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (Talgwu) kimelaani kitendo kikichofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda cha kuwavua madaraka hadharani watumishi wa umma wakisema ni kitendo cha kinyama.
Akizungumza leo Februari 13, 2018 wakati akitoa tamko la chama hicho, Katibu Mkuu, Rashid Mtima amesema chama hicho hakitetei watumishi waovu, bali taratibu zinatakiwa kufuatwa katika kuwawajibisha
Februari 10, 2018 watumishi wa idara za ardhi wa manipaa za Ubungo na Ilala walivuliwa madaraka hadharani hali iliyosababisha mmoja wao, Paul Mbembela (Mkuu wa Idara ya Mipango Miji Ilala) kuzimia kwa muda.
"Tunalaani, tunalaani, tunalaani sana kitendo kilichofanywa na Makonda. Sheria zinataka mtumishi anayekiuka kanuni na sheria za utumishi kushughulikiwa kwa siri hadi uamuzi wa mwisho utakapotolewa,” amesema.
" Jambo baya zaidi tunalolaani hata mtumishi huyo alipozimia Makonda aliendelea kusema Dar es Salaam oyee, huu ni unyama.”
Amesema kibinadamu baada ya Mbembela kuzimia mkutano huo ulipaswa kusimama kwa muda ili kumshughulikia mgonjwa.
Amewaasa wanasiasa na viongozi kufuata sheria wakati wa kushughulikia matatizo ya wafanyakazi.
0 comments :
Post a Comment