Serikali imetangaza msimamo wake kwa watumishi ambao walibainika kuwa na vyeti feki na wale wasiokuwa na vyeti vya kidato cha nne hawana madai yoyote ya kuidai serikali baada ya Rais John Magufuli kutangaza kufanyika kwa uhakiki kwa watumishi wa umma
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji, Sera Mathias Kabundugulu wakati akizungumza kwenye kikao cha kazi cha kujadili masuala ya utawala na rasilimali watu kwa mamlaka za serikali za mitaa, wizara na mikoa ambapo amesema watumishi ambao wamebainika na kuondoka wenyewe, wamefutwa kwenye orodha ya watumishi wa umma na hawana madai wanayodai serikalini ukiwa ndio msimamo.
Kabundugulu amesema pamoja na zoezi kukamilika kwa muda ambao umepangwa, wapo baadhi ya maafisa utumishi wameendelea kuwafumbia macho watu wasio kuwa na vyeti vya kidato cha nne.
0 comments :
Post a Comment