Dkt Magufuli Amwapisha Mwanasheria Mkuu Mpya Na Naibu Wake Leo

Rais Magufuli leo amemwapisha Dk Adelardus Kilangi  kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Paul Ngwembe kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kabla ya uteuzi, Dk Kilangi alikuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (St.Augustine University) kampasi ya Arusha, pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta, (Tanzania Petroleum Upstream Regulatory Authority- PURA).
Naibu Mwanasheria Mkuu Paul Ngwembe kabla ya uteuzi, alikuwa Mkurugenzi wa masuala ya sheria katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (Tanzania Insurance Regulatory Authority-TIRA).
Wateule wote wanatarajiwa kuapishwa Jumamosi asubuhi tarehe 3 Februari 2018.
Awali katika maadhimisho ya Siku ya Sheria, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli katika hotuba yake, aliwanyooshea vidole Waziri wa Katiba na Sheria, Prof Palamagamba Kabudi, na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju na Naibu wake Gerson Mdemu wameshindwa kuandaa kanuni za msaada wa kisheria.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment