Zitto Awaomba Ccm Na Chadema Kusimamisha Kampeni

Kiongozi wa Chama cha ACT-WazalendoZitto Kabwe ameviomba vyama vya Chadema na CCM kusimamisha kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani kwa siku tatu kuomboleza kifo cha mwanasiasa mkongweKingunge Ngombale Mwiru.
"Kingunge  amesaidia kuimarisha CCM na baadaye akasaidia ChademaSioni busara vyama kuendelea  na kampeniNawaomba wasitishe leokesho na Jumatatu mwanasiasa huyu akizikwa wataendelea," amesema Zitto leo Februari 3, 2018 akiwa katika msiba wa mwanasiasa huyonyumbani kwake Kijitonyama, Dar es Salaam.
Vyama takriban 12 vipo katika kampeni za ubunge jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam na Siha mkoani Kilimanjaro. Kampeni hizo zilianza Januari 21 na kutarajiwa kumalizika Februari 16. Uchaguzi katika majimbo hayo na Kata 10 utafanyika Februari 17, 2018.
Kingunge aliyekuwa kada wa CCM mwenye kadi namba naneOktoba 4, 2015 alitangaza kukihama chama hicho na kusema hatojiunga na chama chochote lakini mara kadhaa alionekana akipanda majukwaa ya upinzani kumnadi aliyekuwa mgombea urais wa Chadema na Ukawa, Edward Lowassa kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015.
Mwanasiasa huyo alifariki dunia jana Februari 2, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), anatarajiwa kuzikwa Jumatatu Februari 5, 2018 katika makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Wakati Zitto akieleza hayo, Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais (Utumishi  na Utawala Bora ), George  Mkuchika amesema atamkumbuka Kingunge  kwa mengi.
Amesema alimfahamu Kingunge miaka ya 1970 wakati akiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwamba mwanasiasa huyo mkongwe alikuwa akienda kutoa mihadhara  wakati huo wakiwa wanachama wa Tanu.
“Kifo chake kimenistusha kutokana na mchango wake mkubwa wa kuunganisha vijana,” amesema Mkuchika.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment