Kauli Ya Ridhiwani Baada Ya Kifo Cha Kingunge

Bado watanzania na wanasiasa mbalimbali wapo katika majonzi na maombolezo ya kifo cha mwanasiasa mkongwe ambaye pia amewahi kuwa kiongozi wa serikali Kingunge Ngombale Mwiru ambaye atazikwa leo February 5 2018.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ni moja kati ya wanasiasa waliyoguswa na msiba wa mzee Kingunge na ameamua kutumia ukurasa wake wa instagram kuandika ujumbe huu.
“Nimeamka katika Usingizi nimemkumbuka Mzee Kingunge. Kwangu mimi huyu Mwalimu wa Itikadi ya Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea atabaki kuwa Mwalimu. Najiuliza niandike au niache yabaki kifuani kwangu”
“Iko upande wa nafsi yangu unaniambia niandike kwa yale ninayofahamu kuhusiana na mzee kingunge na huko nafasi unaniambia nisubiri tukuhifadhi kwa nyumba ya milele ili niandike”
“Nitaandika tu……Ulikuwa Mzazi, Mlezi, mtuliza maumivu,rafiki , mcheshi na Uliyeamini katika kile unachokiamini.haukukamilika kama walivyokuwa wengine. ……Nitaandika Ngoja Tukuhifadhi Coming Soon…..Nitaandika”
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment