Magufuli Kuwatunuku Kamisheni Maafisa Wapya JWTZ

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kesho tarehe 03 Februari, 2018 atawatunuku kamisheni maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Watakaotunukiwa kamisheni ni maafisa wapya wa Tanzania na kutoka nchi marafiki waliopata mafunzo katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha.
Tukio la kutunuku kamisheni kwa maafisa hao litarushwa moja kwa moja na vyombo vya habari vya redio, televisheni na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tzkuanzia saa 3:00 asubuhi.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
02 Februari, 2018
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment