Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pius Msekwa amemlilia mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru aliyefariki dunia leo asubuhi Februari 2,2018 Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Akizungumza nyumbani kwake Oysterbay katika mahojiano na Mwananchi, amesema Kingunge amekuwa naye katika shughuli nyingi ikiwamo ndani ya kamati maalumu iliyoundwa na Mwalimu Julius Nyerere kuandaa mwongozo uliotengeneza Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar.
Amesema Kingunge ameshika nafasi mbalimbali za uongozi serikalini ikiwamo waziri wa ushirika na alifanya kazi kubwa kwa vyama vya ushirika.
Amesisitiza kuwa licha ya Kingunge kuondoka ndani ya CCM, lakini ana historia ya kusimamia utengenezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho tawala katika chaguzi nyingi zilizopita.
Msekwa amesema amepokea kifo hicho kwa mshtuko kwa kuwa siku chache zilizopita mwanasiasa huyo mkongwe alifiwa na mkewe Peras.
0 comments :
Post a Comment