Klabu ya Manchester United imefanikiwa kurudi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu England (EPL) kwa kuitafuna klabu ya Chelsea goli 2-1.
Chelsea walikuwa ndio wa kwanza kuliona langu la United kupitia kwa Wilian kunako dakika 32 kabla ya Romelu Lukaku kusawazisha kunako dakika ya 39 na hadi mapumziko timu zote zilikuwa 1-1.
Goli la ushindi la United limefungwa na kinda, Jesse Lingard kunako dakika ya 75 hadi filimbi ya mwisho inalia, Man United 2 Chelsea 1.
0 comments :
Post a Comment