Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), Emmanuel Mwakasaka ameonyesha hofu kuhusu usalama wa wabunge bungeni kutokana na viti kuwa vibovu.
Ametoa mfano akisema amewahi kuanguka baada ya kukalia kiti kibovu.
Mwakasaka ametoa kauli hiyo bungeni leo Februari 2,2018 baada ya kuomba mwongozo wa Spika.
Amesema viti wanavyokalia vingi ni vibovu, vimefumuka na baadhi kung’oka hivyo kuwa hatari kwa wabunge kwa kuwa vinaweza kuwategua nyonga.
"Hivi ninavyoongea pale nyuma anapokaa mheshimiwa Obama (Albert- Mbunge Manyovu-CCM) hakuna kiti, nimebinuka nacho mimi. Isingekuwa mazoezi kisogo changu kingekuwaje? Pale kiti kipo chini nimeanguka nacho mimi,” amesema.
Amesema, "Naomba mwongozo wako hivi viti vinafanyiwa matengenezo wakati gani? Hasa kwa kuangalia usalama wa wabunge kwa kuwa wengine ni watu wazima wakiteguka nyonga itakuwaje?”
Akijibu, Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge amesema mwongozo huo umepokewa na wataona ni nini cha kufanya kulingana na hali ya fedha.
0 comments :
Post a Comment