Leo February 18, 2018 Mwenyekiti wa mtandao wa Wanafunzi Tanzania, Abdul Nondo amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kujiuzulu kutokana kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji NIT. Pia kama atashindwa basi Rais amtengue.
“Tunamuomba Waziri wa Mambo ya Ndani, ajiuzulu kwa sababu ameshindwa kusimamia nafasi yake na kuangalia mienendo ya Jeshi la Polisi ambapo kila siku matukio yanatokea,” -Nondo
“Haya matukio yamekuwa yakishamiri sana ambapo yalianzia kwa wanasiasa, ambapo tulikuwa tukiyasikia haya matukio hadi kwa wanafunzi na watu wasiokuwa na hatia,” -Nondo
0 comments :
Post a Comment