Chadema Yatoa Tamko Baada Ya Uchaguzi Marudio


JANA February 18, 2018 Kumefanyika uchaguzi wa marudio katika Majimbo Mawili Jimbo la Siha na Kinondoni ambapo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa taarifa yake kuhusu mwenendo wa uchaguzi wa marudio uliofanyika February 17, 2018 katika Jimbo la Siha na Kinondoni.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Vicent Mashinji imeeleza kuwa baada ya upigaji wa kura katika uchaguzi kumalizika uligubikwa na vitendo vya viovu vya kihalifu.
CHADEMA imeeleza kuwa katika Jimbo la Kinondoni Tume imefanya urasimu kinyume cha sheria na kumefanyika makosa ya makusudi kuhakikisha chama hicho hakiweki Mawakala kwenye vituo vya kupiga kura kwa zaidi ya saa 2 tangu vituo vilipofunguliwa.
Katika Jimbo la Siha CHADEMA imeeleza kuwa vyombo vya Dola, hususani Jeshi la Polisi limetumika kubadili matokeo kwa kuwalazimisha Mawakala kusaini fomu za Matokeo tofauti na fomu rasmi zilizoko vituo na huku wakitumika kupora Masanduku na kubandika matokeo yasiyojulikana yametoka wapi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment