Tamko La IGP Kwa Wananchi

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, ameitaka jamii pamoja viongozi wa dini kushirikiana na Polisi ili kutokomeza makosa mbalimbali katika jamii ikiwemo, mauaji yatokanayo na wivu wa mapenzi, ulevi, ubakaji ili kuiweka nchi salama zaidi.
IGP Sirro ameeleza hayo leo Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa takwimu za sasa zinaonyesha matukio ya aina hiyo yamekithiri sana nchini Tanzania jambo ambalo jamii inapaswa kubadilika ili kupunguza matukio hayo.
"Kuna makosa ambayo watu lazima wabadilike na hili haliitaji Jeshi la Polisi maana mimi nasimamia  Sheria lakini kuna viongozi wa dini wazungumzie hayo mambo. Muumini wako akija Kanisani au Msikiti na ukimwambia katazo la Mungu anaweza akabadilika", alisema IGP Sirro.
Kwa upande mwingine, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Sirro amesema kuna makosa ambayo viongozi wa dini wakishiriki kwa ukaribu zaidi inaweza kupunguza huku akiitaka jamii kubadilika kitabia ikiwemo kuachana na ulevi wa kupindukia.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment