Kufuatia kifo cha mwanasiasa Mkongwe nchini, mzee Kingunge Ngombale Mwilu kilichotokea alfajiri ya leo,watu wanataka kufahamu namna mazishi ya mzee huyo yatakavyo fanyika.Hiyo ni kutokana na mzee huyo enzi za uhai wake kusema kwamba hana dini.
Ndugu wa karibu wa marehemu,Balozi Ally Mchumo ambae ni msemaji wa familia amesema kwamba utaratibu wa namna mzee Kingunge atazikwa utajulikana siku ya mazishi.
Mzee kingunge anatarajiwa kuzikwa siku ya jumatatu katika makaburi ya Kinondoni jijini Dare es salam.
0 comments :
Post a Comment