TARATIBU ZILIZOWEKWA KUMUONDOA ZUMA MADARAKANI.


Image result for jacob zuma
Kiongozi wa chama tawala cha African National Congress (ANC) nchini Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, amesema anazungumza moja kwa moja na Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma, kujadili masharti ya kujiuzulu na kuhakikisha mabadiliko katika uongozi wa taifa hilo.
Chama cha ANC kinatafuta "njia yenye heshima" kwa Jacob Zuma, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2009, na anaendelea kukabiliwa na madai ya kashfa kadhaa za rushwa na ufisadi. Muhula wke kawaida unamalizika katikati ya mwaka 2019.
Shinikizo kwa Rais Zuma limeongezeka tangu Cyril Ramaphosa achaguliwe kuwa kiongozi wa chama cha ANC mwezi Desemba.
Katika taarifa, Cyril Ramaphosa amesema kuwa alikutana na Rais Zuma kwa mara ya kwanza siku ya Jumanne mjini Cape Town, na wanatarajia kukamilisha majadiliano yao na kutoa ripoti kwa taasisi za ANC "katika siku zijazo".
Mchakato huo unapaswa kutatua hali inayoendelea bila kusababisha vurugu au mgawanyiko nchini, Bw Ramaphosa ameongeza.
Mtandaoni wa Times Live umeripoti, ukinukuu chanzo kutoka kilio karibu na utawala nchini Afrika Kusini, kwamba Rais Zuma atajiuzulu kama orodha ya masharti aliyoyatoa itakua imekubaliwa.
Siku ya Jumapili usiku Jacob Zuma, mwenye umri wa miaka 75, alikutana kwa mazungumzo na maafisa wakuu sita wa bodi ya uongozi ya chama cha ANC katika makazi yake rasmi mjini Pretoria, lakini matokeo ya mkutano huo hayakujulikana.
Si mara ya kwanza kwamba rais wa Afrika Kusini anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu. Mnamo mwaka 2008, baada ya kuchaguliwa kwake kama kiongozi wa ANC, Jacob Zuma alihusika katika utaratibu wa kumuondoa madarakani Thabo Mbeki.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment