Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Godwin Ngwilimi amepongeza Rais John Magufuli kwa kutekeleza matarajio ya watanzania.
Ngwilimi ametoa kauli hiyo leo Februari mosi jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha Maadhimisho ya 22 ya siku ya Sheria na uzinduzi wa mwaka mpya wa kimahakama.
Pia, ameomba uwezeshaji wa rasilimali fedha katika muhimili wa mahakama ili kushughulikia changamoto zinazoikabili. "Kama chama cha mawakili, tunakuunga mkono na tunaahidi kutoa ushirikiano kwa mahakama pale inapostahili."
Ametoa wito akisema, watumishi wa mahakama, majaji, wasajili, watendaji , makarani na watumishi wengine, mawakili, wanasheria popote walipo wanatakiwa kutambua mwelekeo wa nchi unabadilika kwa kasi, matarajio ya wananchi , kuondokana na utamaduni wa kuendelea kufanya kazi kimazoea, kutumia fursa zilizopo ikiwamo Tehama ili kuboresha huduma kwa wananchi.
Pia kuendelea kusimamia maadili ya kitaaluma na uadilifu , hata Mungu anapenda uadilifu na imeandikwa katika vitabu vitakatifu, kulinda na kuhifadhi misingi ya kitaaluma na kujifunza kwa kufuata makosa yaliyotokea hapo nyuma
Ngwilimi ametoa wito akisema: " Kama sehemu ya watanzania, tusitumie mahakama vibaya, kusumbua wengine, kuonea wengine, kama sehemu ya majaribio, siyo maabara , kama jumba la kamari.
0 comments :
Post a Comment