Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Mkazi Angelina Mabula amesema ni marufuku halmashauri kuchukua maeneo ya wananchi bila ya kuwalipa fidia.
Mhe. Mabula amesema hayo Wilayani Butiama mkoa Mara wakati wa ziara yake yenye nia ya kutatua migogoro ya ardhi pamoja na kukagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi.
Amesema wakati wa mchakato wa kuchukua maeneo ya mwananchi ni vyema wahusika wakashirikishwa kuanzia hatua ya awali sambambana na kuelimishwa juu ya zoezi hilo ili kuepuka migogoro inayoweza kutokea.
‘’Cha msingi ni kuanza kuzungumza na mwananchi kabla ya kuchukua eneo lake na kumueleza eneo ambalo ataachiwa na halmashauri zihakikishe mwananchi huyo anapimiwa pamoja na kupatiwa hati yake’’ alisema Mabula
Aidha, mhe. Mabula amesema eneo litakalochukuliwa na halmashauri viwanja vyake kuuzwa fedha itakayopatikana halmashauri ihakikishe inatumika katika kutengeneza miundo mbinu na huduma nyingine za jamii na kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo migogoro haiwezi kutokea.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ameziagiza halmashauri kuhakikisha zinapanga miji kulingana na ‘master plan’ ili kuwa miji bora iliyopangika
0 comments :
Post a Comment