Makonda aagiza mwanafunzi aliyepotea ashughulikiwe

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amelitaka jeshi la polisi kuendelea kufanya kazi bila kutetereshwa na mtu yeyote na amemuagiza Kamanda Mambosasa na timu yake kuwashughulikia watu wanaotumia lugha za kashfa dhidi ya viongozi wa nchi ambao ni nembo ya taifa.

Pia amewaomba waandishi wa habari kuangalia taarifa wanazozisambaza kwa umma kuhakikisha kuwa ni taarifa ambazo zimethibitishwa na mamlaka husika kwani taarifa nyingi zinazosambazwa zimekuwa zikileta taharuki katika umma.

Hayo ameyasema kufuatia habari zilizosambaa hivi karibuni kuhusu Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini Tanzania ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Abdul Nondo ambaye alipotea siku chache zilizopita na kupatikana akiwa Mafinga.

Amesema kuwa kitendo cha waandishi wa habari kuandika habari ambazo hazijathibitishwa na mamlaka husika huchafua mkoa wa Dar Es Salaam na hivyo ameagiza kijana huyo ashughulikiwe.

”Juzi nimesikia kuna mmoja amesema ametekwa, mi nafikiri wakimalizana nae kule Iringa watuletee huku Dar es salaam, asituchafulie mkoa wetu” amesema Makonda.

Aidha ameomba Mamlaka ya Mawasiliano TCRA, kushughulikia makosa ya kimtandao ili kuhakikisha nchi yetu inabaki katika amani na utulivu,.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment