Mwanaume mmoja nchini Uingereza amezua gumzo baada ya kupimwa na madaktari na kukutwa na ugonjwa wa kisonono katika kiwango cha juu na kibaya zaidi kuwahi kutokea duniani.
Inaelezwa kuwa mwanaume huyo alikuwa na mpenzi mmoja akiwa nchini Uingereza lakini aliupata ugonjwa huo baada ya kukutana kimwili na mwanamke kutoka Kusini Mashariki mwa bara la Asia.
Madaktari wameeleza kuwa mwanaume huyo alipata maambukizi hayo tangu mwanzoni mwa mwaka huu na hadi sasa ugonjwa huo umeshindwa kutibika.
Maafisa afya tayari wameshaanza kutafuta wanawake wengine ambao yawezekana wamekuwa na uhusiano na mwanaume huyo ili pia waanze kusaidiwa
0 comments :
Post a Comment