Kocha mkongo atua Dar kuchukua mikoba ya Lwandamina Yanga

Yanga imemtwaa kocha Mwinyi Zahela kumridhi Kocha George Lwandamina.

Tayari kocha huyo yuko nchini na taarifa zinasema anatarajia kumalizana na uongozi wa Yanga, hii leo.

Mmoja wa wanakamati wa Yanga, amesema kocha huyo alikuwa katika kikosi cha timu ya taifa ya DR Congo iliyokuja nchini kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Taifa Stars na kulala kwa mabao 2-0. 
Kocha Mkuu wa DR Congo kwa sasa ni Florent Ibenge aliyewahi kuifundisha AS Vita, moja ya timu kubwa na kongwe nchini humo.

“Tayari ametua nchini jana, nafikiri atamalizana leo na uongozi tayari kwa kila kitu na ataanza kazi,” kilieleza chanzo.

Yanga ilikuwa chini ya Noel Mwandila na Shadrack Nsajigwa ambao walikuwa wakishikilia mikoba ya Lwandamina aliyeamua kurejea kwao
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment