Hivi juzi msiba wa mwanadada masogange umezua mambo mengi sana mapya ambayo mengine yalikuwa hayajulikani lakini yalijulikana na mengine yalikuwa hayafanyiki lakini yaliweza kufanyika.
kuna picha ilisambaa ikimuonyesha msanii wa maigizo rammy akiwa amezimia huku akiwa ameshikilia kitambaaa chake mkononi na watu wengi kuhoji kwanini msanii huyo aliweza kuzimia na kuweza kupata nguvu ya kushikilia kitambaa.
Moja ya watu waliomshambulia Rammy kwa tukio hilo alikuwa Irene paul ambae alisema kuwa Rammy amekuwa akiigiza mambo hayo katika msiba huo ili kuonekana kama ameguswa sana ilihali sio kweli
Inasemekana eti kwamba wasanii hawa hawaelewani kabisa, na kwamba hata kazini wanashindwa kufanya kazi pamoja kwa sababu ya tofauti zao.
Kwa habari zisizothibitika lakini zinazosambaa chinichini ni kwamba Irene na Rammy walishawahi kugombana mpka akutaka kurushiana ngumi walipowahi kuwa katika moja ya locationzao za kazi.
Maswali yalizidi kuwa mengi kwa mashabiki wa wasanii hawa hasa baada ya irene kuweka picha ya galis na kutoa mapovu lakini aliamua kufunga sehemu ya maoni ili mashabiki wanaomfuata wasiweze kuandika chochote hivyo jhii imezua gumzo zaidi.
Hata hivyo baada ya kuchunguzwa kwa taarifa za kuzimia kwa Galis, wataalamu wanasema kuwa inawezekana kabisa mtu, kuzimia, kufa au kuishiwa nguvu lakini akaweza kushikilia kitu mkononi kwa muda .
0 comments :
Post a Comment