Kesi ya Tido yapigwa kalenda Hadi June 8

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, itaendelea kusikiliza ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka Juni 8 huu katika kesi inayomkabili Mkurugenzi mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando.

Wakili wa Takukuru, Leonard Swai jana amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa  kesi  inayomkabili Tido leo ilipaswa kuendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa  mashahidi wa upande wa mashtaka.

Lakini shahidi waliyemtarajia kutoa ushahidi katika kesi hiyo ana udhuru.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Shaidi ameiahirisha kesi hiyo hadi Juni 8 ili mashahidi wa upande wa mashtaka waendelee kutoa ushahidi.

Katika kesi hiyo tayari mashahidi watatu wa upande wa Jamhuri wamekwishatoa ushahidi .

 Mashahidi hao ni  Ofisa uchunguzi wa Takukuru, Victor Lesuya, Mwanasheria wa TBC, Gwakisa Mlawa na Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TBC, Clement Mshana.

Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh887.1 milioni
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment