Waitara Amtaka Spika Kuwapatia Wabunge Laptop

Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema), amemuomba Spika wa Bunge, Job Ndugai alieleze bunge ni lini atawagawia wabunge kompyuta mpakato (laptop) ili wasiendelee kutumia nyaraka za makaratasi wakati wa shughuli za bunge.

Amesema ugawaji wa laptop hizo kwa wabunge ni moja ya ahadi iliyotolewa na Spika Ndugai kama sehemu ya mkakati wake wa kuliboresha bunge.

Waitara ametoa hoja hiyo bungeni leo Mei 18, alipokuwa akiomba mwongozo wa Spika akitumia kanuni ya 68 (7).

Akijibu mwongozo huo, Spika Ndugai amesema atalitolea majibu suala hilo baadaye
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment