Rais wa Marekani, Donald Trump ametilia shaka kuhusu kufanyika kwa mkutano na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un mwezi june mwaka huu huko Singapore.
Ameyasema hayo mara baada ya Korea Kaskazini kutishia kujiondoa katika mkutano huo endapo Marekani itaendelea kusimamia msimamo wake wa kuiwekea vikwazo nchi hiyo.
Aidha, Rais Trump hakuweka wazi ni masharti gani ambayo yamewekwa kwa ajili ya mkutano huo,na alipoulizwa na waandishi wa habari juu ya masharti aliyoiwekea Korea Kaskazini amesema kuwa suala la kuachana na silaha za nyuklia ni lazima litekekelezwe na Korea Kaskazini.
Mkutano kati ya rais Trump na Kim Jon-un uanatarajiwa kufanyikwa June 12 nchini Singapore ukitanguliwa na mkutano wa marais wa Korea hizo mbili uliofanyika mwezi April.
Hata hivyo, ameongeza kuwa mwelekeo wa Kim Jong-un umebadilika baada ya ziara yake ya pili mwezi huu nchini China
0 comments :
Post a Comment