ALIYEKUWA mshambuliaji wa Lipuli FC ya Iringa, Adam Salamba amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Klabu ya Simba kwa dau la Shilingi milioni 30.
Simba wameinyaka saini ya Salamba baada ya kuwazidi kete Yanga na Azam waliokuwa wakimuwania mchezaji huyo.
Salamba amesaini mkataba huo mbele ya Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ na baadaye kukutana na Mohamed Dewji, Bilionea anayetarajia kuwekeza ndani ya Simba kitita cha Sh bilioni 20.
0 comments :
Post a Comment