Kubenea: Mbunge CCM Akikwamisha Bajeti Hii Nisilipwe Mshahara

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), amesema kama atatokea Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi CCM) akakwamisha bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ataruhusu mshahara wake asilipwe.

Amesema pamoja na kwamba baadhi ya wabunge wa CCM wanaonyesha kutoridhishwa na baadhi ya bajeti za wizara lakini hawana uwezo wa kuzuia bajeti kwa kuwa wanazuiwa na chama chao kufanya hivyo.

Kubenea ameyasema hayo bungeni leo alipokuwa akichangia bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/19.

Katika hatua nyingine kubenea ameliambia bunge kwamba anatarajia kuwasilisha hoja binafsi bungeni akitaka bunge liunde kamati maalumu kuchunguza operesheni sangara inavyotekekezwa katika Ziwa Victoria.

“Operesheni hiyo lazima ichunguzwe kwa sababu imeumiza wavuvi na wananchi kwa ujumla,” amesema.

Naye Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa (CCM) amesema matatizo yaliyoko nchini yamesababishwa na baadhi ya wataalamu ikiwamo kupiga chapa mifugo huku wakijua wanaharibu ngozi
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment