Mbunge wa Kahama Mjini, Jumanne Kishimba (CCM), amesema kuna haja ya serikali kusitisha ulaji wa samaki nchini kama uvuvi wa samaki hautakiwi.
Amesema pamoja na kwamba serikali inapiga vita kupitia operesheni sangara katika Ziwa Victoria, operesheni hiyo haiwezi kukubaliwa kwa sababu inaumiza wavuvi.
Kishimba ameyasema hayo bungeni leo alipokuwa akichangia bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya mwaka wa fedha wa 2018/19.
“Mji wa Mwanza umejengwa kupitia pamba na madini, na hao samaki wanaopigwa marufuku kuvuliwa nao wamechangia kwa sehemu kubwa ukuaji wa mji huo naiomba serikali iwagawie wavuvi vifaranga wa samaki ili zao la samaki liweze kuinufaisha serikali na wananchi kwa ujumla,” amesema
0 comments :
Post a Comment