Mahakama yaondoa zuio matumizi ya kanuni za maudhui ya kimtandao

Mahakama Kuu ya Mtwara imeondoa mahakamani shauri la kupinga  matumizi ya Kanuni za Maudhui ya Kimtandao (Online Content Regulation) lililofunguliwa na Kituo cha Sheria na  Haki za Binadamu (LHRC) na wenzake dhidi ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Mbali na LHRC wengine waliopeleka zuio hilo ni Tanzania Human Rights Defenders (THRD); Baraza la Habari Tanzania(MCT) na Jamii Media; Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa ); na Jukwaa la Wahariri (TEF).

Kanuni hizo zilipaswa zianze kutumika Mei 5 lakini mahakama hiyo ikaweka zuio la muda Mei 4, baada ya kuwasilishwa kwa shauri la kupinga mahakamani hapo.

Kesi hiyo namba 12/2018 ilisomwa jana Mei 28 mbele ya Jaji Mfawidhi, Dk Fauz Twaib na ilipangwa kutolewa  uamuzi juu ya mapingamizi matatu yaliyowasilishwa na upande wa Serikali.

Akitoa uamuzi huo jana, Jaji Dk Twaib alisema mahakama hiyo imekubali pingamizi moja kati ya matatu yaliyowasilishwa; kwamba mashirika yaliyopeleka kesi mahakamani hapo hayana maslahi ya kutosha kwa maana ya kufungua shauri hilo na kwamba hawakuonyesha  namna moja kwa moja yatakavyoguswa na kanuni hizo.

Hivyo, mahakama iliondoa shauri hilo lakini inatoa nafasi kwa mashirika hayo kama yatahitaji kupeleka shauri lingine kama watajidhihirisha wana nafasi ya kufanya hivyo.

Credit: Mwananch
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment