Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amelieleza bunge jinsi operesheni sangara ilivyofanyika kwa mafanikio katika Ziwa Victoria licha ya malalamiko juu ya utekelezaji wake.
Kutokana na hali hiyo Mpina pia amewataka wabunge kumuunga mkono kwa kuwa kazi wanayopambana nayo ni nzito na inahitaji ushirikiano.
Amesema mafanikio yaliyopatikana katika operesheni hiyo ni pamoja na idadi ya samaki kuongezeka.
Akihitimisha bajeti ya wizara yake aliyoiwasilisha bungeni jana jijini Dodoma leo, Mpina amesema wakati wa utekelezaji wa operesheni hiyo wamefanikiwa kukamata nyavu haramu 555431, kilo 181217, mabondo kilo 5147,pikipiki 269, na pia magari 564 yalikamatwa.
“Pamoja na wabunge kulalamikia operesheni sangara hakuna mbunge hata mmoja aliyewahi kunipa ushahidi wa jinsi wavuvi wanavyonyanyaswa kupitia operesheni hiyo,” amesema Mpina.
Akithibitisha jinsi operesheni hiyo inavyofanyika vizuri amesema wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa hivi karibuni wilayani Ukerewe, hakukuwa na malalamiko yaliyotolewa na wananchi
0 comments :
Post a Comment