Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewapongeza Wabunge kwa kuvaa Kanzu kwa wingi na kwa Wabunge wa Kike kuvaa Hijab.
Spika ametoa pongezi hizo leo, Mei 18 mapema katikati ya kipindi cha maswali na Majibu kwa serikali ambapo pia amemsifia Naibu Spika wa Bunge kwa kuvaa Baibui na Hijab.
“Wabunge kama hatujaendelea nimefanya utafiti wangu leo watu wengi sana wamependeza kwa kuvaa Kanzu na kofia hongereni sana, tukumbuke tu kanuni tunapo vaa tunatakiwa ivaliwe vilevile kama inavyovaliwa Pwani na miguu sio kuvaa kiatu cha kamba hapana unavaa kobazi,” amesema Spika Ndugai huku akicheka na Wabunge wakimpigia makofi.
“Lakini kwa upande wa kina mama leo Hijab zimekubali, lakini katika Hijab, Hijab namba moja leo hii ni ya Naibu wangu Mh. Naibu Spika, Mh. Naibu Spika ebu simama kidogo hapo ahsante sana, hiyo inaonyesha Utanzania wetu sisi ni wamoja,” ameongeza Spika
0 comments :
Post a Comment